Kwa Nini Watu Wengi Huasita Kuanza Ujenzi?

Ni Kiasi Gani Cha Fedha Kinatosha Kuanza UjenziWateja wengi hutupigia wakituuliza bajeti ya kuanzia. Wengi wana viwanja tayari lakini wanasita kuanza kwa kuhofia bajeti ndogo. Ukweli ni kwamba kumiliki kiwanja tayari ni hatua kubwa sana unayoianza katika safari ya ujenzi.


Je, Kuna Bajeti Maalum ya Kuanza Ujenzi?

Gharama ya kuanza ujenzi hutofautiana kulingana na ramani ya nyumba, aina ya ujenzi unaotaka, jinsi kiwanja kilivyo kama ni tambarare au mlimani, bei za materials katika eneo lako na mambo mengine ambayo hujitokeza kwenye site. Hakuna kiasi kimoja kinachotumika kwa kila mtu kwa sababu kila mradi una uhalisia wake.

Unaweza Kuanza Hata Kama Bajeti Ni Ndogo

Habari njema ni kwamba ujenzi unaweza kuanza hatua kwa hatua. Sisi Jenga Real Estate tunajenga kulingana na uwezo wako. Unaweza kuanza na msingi, ukakusanya fedha nyingine, halafu tukaja kuinua boma. Njia hii husaidia kupunguza presha na kukupa nafasi ya kupanga vizuri matumizi yako.

Kwa Nini Uchague Jenga Real Estate?

Kama unahitaji mafundi wa ujenzi, interior design, exterior design au finishing ya nyumba au jengo la biashara, tuko tayari kukusaidia. Tunafanya kazi safi sana, nyooka, kwa gharama rafiki na kwa kasi inayookoa gharama zisizo za lazima. Pia tunatoa ushauri bila malipo ya ziada ili kuhakikisha unafanya maamuzi sahihi kwenye kila hatua ya mradi wako.

Tembelea Site Zetu Ujionee

Tunaweza kufika kwenye site yako kukushauri, au kama unataka kuona ubora wetu moja kwa moja, unaweza kutembelea site ambazo mafundi wetu wanafanya kazi kwa sasa ili uone jinsi kazi zinavyonyooka.

Ofisi zetu zipo Kisasa Dodoma na tunafanya kazi nchi nzima.

Wasiliana Nasi Sasa

📞 Piga simu: +255 741 422 186

💬 WhatsApp: +255 712 592 186

Karibu sana.

Pages